Mtafsiri:
Innocent Zephania
Manyerere Jackton, ambaye mpaka sasa ameshaandika makala
zaidi ya ishirini kuwatuhumu Wamasai wa Loliondo akidai kwamba ni waharibifu
kutoka Kenya ambao asasi yao ya kiraia inawavuruga wawekezaji, hivi sasa
ameandika tena kuhusu mimi… Ni Manyerere huyu huyu ambaye mwanzoni alikwenda
mbali zaidi akidai kwamba zaidi ya asilimia 70 ya watu wa Loliondo ni ‘Wakenya’
na kwa kutaka kuthibitisha hilo, akachapisha orodha ya majina aliyodai ni ya
‘Wakenya’ hao. Msingi hasa wa makala yake, kabla ya hii ya sasa aliyoandika
kuhusu mimi, makala aliyoiandika katika Gazeti la Jamhuri, June 15, 2016 yenye
kichwa cha habari “Atuzwa kwa kuisumbua Serikali” (akiwa ameshirikiana na watu
wawili wanaosadikika kuwa walarushwa wakubwa wa Loliondo) ni kutaka kumchafua mwanaharakati Maanda Ngoitiko tena kwa kutumia hoja za kizushi na za
kuunganisha unganisha kuhusu namna ambavyo anadai nimefanya kazi chini ya asasi ya mwanaharakati huyu kitu
ambacho sijawahi kufanya kwa namna yeyote ile, na hata kama ningekuwa
nimeisaidia kwa namna nyingine, Je hilo sio jambo jema? Kilichotokea katika
makala yake ya mwisho ni kwamba, Hashim Shaibu Mgandilwa - asiye na uadilifu,
aliyekuwa mkuu wa wilaya - ni lazima angepokea maombi yangu kwa ufupi kuhusu
kubatilisha hadhi ya marufuku ya kusafiri (prohibited immigrant status), kwa
Waziri wa mambo ya ndani aliyejiuzulu Kitwanga kisha apeleke kwa mwandishi huyu
anayeipinga Loliondo. Akiwa katika mtandao wa kijamii, kwa kejeli, Hashim
Shaibu Mgandilwa akaniambia “nimesikia
unataka unataka ku revoke PI njoo nikusaidie” na kwa muda mfupi sana baada
ya kuniandikia hivyo, Manyerere Jackton naye akanitumia barua pepe ikiwa na
ujumbe wa kitoto unaoishia na maneno haya “Finally,
you will know who is the worst journalist and who is the worst mzungu!”
kumaanisha kwamba “Mwishowe utapata kujua
kwamba yupi ni mwandishi mbaya sana na yupi ni mzungu mbaya sana” huku
akiwa ameambatanisha na nakala ya barua yangu ya kwanza niliyowahi kutuma
kuomba kubatilishiwa marufuku ya kusafiri (prohibited immigrant status).
Angeweza kupata pia vielelezo vyangu vingine kuhusu maombi yangu kwa kina,
lakini kwa kuwa ni mvivu pia au labda hakutaka basi hakuweza kufanya hivyo.
Katika makala yake toleo la mtandaoni, makala ambayo haina hata jina la
mwandishi - Manyerere alidai kwamba ni kutokana na “uchunguzi” uliofanywa na
Gazeti la Jamhuri, hatimaye wamefichua hayo maombi yangu ya kutaka
kubatilishiwa...
Ni jambo la kustaajabisha sana kuona kwamba, kwa nini
Gazeti la Jamhuri linaendelea kuchapisha tuhuma za upotoshaji dhidi ya jamii ya
Wamasai wa Loliondo ambao ni Watanzania. Kwa kumzingatia Manyerere binafsi,
nimefikiri sana pengine atakua na mapungufu ya kisaikolojia, lakini kwa
kuzingatia pia msingi wa niliyoyadadisi, inaonekana wazi kwamba mwandishi huyu
anafadhiliwa na watu wa kitalu cha uwindaji cha OBC, watu wa
ngazi ya juu kabisa wa jamii ya Falme za Kiarabu (UAE). Suala hili limejirudia rudia mpaka kupelekea
serikali ya Tanzania kushawishika kutangaza uvamizi wa ardhi katika eneo hilo
na mwaka 2009 ikawahamisha kwa nguvu, kutoka kilometa za mraba 1,500 (sehemu
yote ni ardhi ya kijiji), bila hata ya ridhaa ya mahakama, Wamasai hao wa
Loliondo. Kwa namna yeyote ile, makala ya hivi karibuni ya mwandishi huyu si ya
kiuadilifu na imejaa simulizi za kizushi kwa nia ya kuudhi. Manyerere alipata
pia kuandika bila weledi baada ya mimi kushikiliwa kinyume cha sheria nikiwa
Loliondo kwa siku tatu bila ya kuruhusiwa kuwasiliana na mtu yeyote mnamo mwaka
jana. Niliandika hivi katika blog baada ya kuachiwa huru.
Manyerere aliendeleza kutokuwa na weledi kwa kuandika
kwamba nilikamatwa nikiwa napata chakula cha jioni katika hoteli aliyoitaja kwa
jina la “Onesmo” hotel kitu ambacho sio kweli kwani hakuna hoteli yenye jina
hili huku ilihali mimi nilikuwa katika nyumba ya kulala wageni ya ‘Honest Guest
House’. Ijapukuwa ni dosari ndogo lakini ina msingi...
Manyerere alimtaja aliyekuwa Mkuu wa Wilaya (aliyehamishiwa
Kigamboni) kama mtu ambaye amenifafanua mimi kuwa mdau mkuu katika kuiharibu
Loliondo na Serengeti, na hii ikawajengea msingi…
Pia mwandishi huyu, anaikuza mada kwa hoja kwamba
nilipata hifadhi Oloip, katika nyumba ya kulala wageni inayomilikiwa na aliyekuwa
mbunge Mh Timan ambaye mke wake ndiye mwanaharakati pekee wa Loliondo ambaye ni
mzaliwa wa Kenya, kitu ambacho kinamfanya mwanamama huyu kukosa nguvu kiasi
kumpinga Manyerere. Ijapokuwa Manyerere hakufanikiwa sana kwa hilo kwa vile
mwanamama huyo hana wadhfa tena wa udiwani wa CCM na mwaka jana kwenye
uchaguzi, amechaguliwa Diwani wa viti maalumu wa Chadema. Manyerere aliendelea
kudanganya kwamba nimeonekana kwenye mkutano wa siri huko Kirtalo nikiwa na Mh
Tina Timan, japo nilishamfafanulia Manyerere kwa ufasaha kabisa mwaka jana
kwamba si huyo mwanamama, bali ni watu wengine kabisa niliokutana nao huko
Kirtalo nikiwa natimiza haki yangu ya msingi kama binadamu ya kukutana na watu
wengine na kuchanganyika kwa hiari kwa ajili ya kutoa mawazo yangu hadharani.
Mwandishi huyu tena anarudia kupotosha kwamba nimekusanya
“mabilioni ya fedha” kutoka katika mashirika ya kimataifa bila kuzingatia hoja
kwamba sijawahi kuchangisha shilingi ya kitanzania. Labda abainishe wazi kwamba
nani katika dunia hii amenipatia fedha. Kwa kuwa mwandishi huyu anaandika tu
bila kuwa na mipaka ya kitaalamu, ni rahisi kwake kuandika chochote kile kuhusu
uhatari wa wazungu na wamagharibi na kwa namna wanavyonimwagia fedha...
Hupendelea kutumia muda mwingi kutunga uongo wa mimi na mambo ya fedha jambo
ambalo linanifanya nifikiri sana kwamba pengine anafadhiliwa na OBC
Uongo mwingi ambao nimeshaukanusha tangu mwaka jana bado
unarudiwa rudiwa, kama yale madai ambayo hayana maana ya kusema kwamba wakati
niliposhikiliwa kinyume cha sheria, nilidai kwamba endapo serikali ya Tanzania
itaendelea kunifuatafuata, nitahakikisha Sweden inakatisha misaada yake nchini.
Manyerere anajua fika kwamba sikusema kitu kama hicho, na ni kwa sababu pia
sina ushawishi katika hilo, lakini ni kitu tu ambacho “mwandishi” anapenda
kukiandika. Kitu nilichowaambia wale mbumbumbu katika kituo cha polisi - wale
wote isipokuwa mmoja, hawakujitambulisha kwangu, Mkuu wa Wilaya alikuwepo
lakini nilimtambua - niliwaambia walipaswa kumshikilia pia meneja wa mashirika
ya nje ambayo yanakiuka haki za ardhi - OBC kwa kuwa tishio dhidi ya kilomita
za mraba 1,500, na pia Thomson Safaris - kutoka Marekani, kwa kuhusika na
umiliki kinyume wa ekari 12,617, ardhi ya Wamasai. Watu wanaofichua ukweli
kuhusu makampuni haya, si watu sahihi wa kukamatwa. Pengine ni Manyerere
mwenyewe aliyetunga uongo huu au alitumia vyanzo vyake vya siri vya
kimbumbumbu. “Majibizano” niliyoyapata kutoka kwa watu katika kituo cha polisi
cha Loliondo ni kwamba “hakuna nchi
katika dunia hii, mgeni anaruhusiwa kuzungumza siasa na watu” kauli
inayoonyesha ujinga uliokithiri kuhusu haki za binadamu za msingi kama vile
uhuru wa mtu kujieleza na kutoa maoni yake na uhuru wa kuchanganyika na watu
kwa hiari.
Nimekua nikijihusisha na kuandika katika blog kuhusu uporaji
wa ardhi unaofanywa na wawekezaji ndani ya Loliondo kwa takribani miaka sita
sasa, sababu kubwa ikiwa kwamba nilikutana na mkasa ukaja ukazimwa kwa uongo na
nikapata misukosuko wakati nilipokwenda Loliondo kuona kwa macho yangu
mwenyewe. Sasa kama hakuna wa kushughulika nalo, nitafanya kila linalowezekana
na kwa muda mrefu kama itakavyowezekana. Manyerere kwa upande mwingine anatumia
nafasi katika gazeti la kitaifa, si tu kwa kumchafua mwanaharakati yeyote
ambaye anaonekana kwenda kinyume na hawa wawekezaji, bali pia kuwabeza baadhi (asilimia 70) ya wakazi wa Loliondo.
Anatumika kama silaha ya ukoloni mamboleo unaounga mkono uharibifu, suala
ambalo ninalifichua na kulisemea kwa sasa. Dhana hii inajifafanua pia pale
ambapo anatumia hata maneno ya kibaguzi kama “mzungu” yanayotumika mtaani, yeye
huyatumia kwenye vichwa vya habari vya magazeti. “Kosa” kubwa analoweza
kulibaini kwangu ni rangi yangu ambayo amekua akiitafakari kila mara huku
akiwawezesha walioko nyuma yake kupaza sauti kuhusu nchi za magharibi asijue
kwamba binafsi ninataka kuiimarisha nchi ya Tanzania kwa kuwaunga mkono
wapigania haki ya ardhi ya Wamasai. Watanzania wengine wanaonishambulia kwa
rangi yangu ni wale walioajiriwa na hawa wawekezaji waporaji wa ardhi, na wale
wanaofurahia ubaguzi dhidi ya kundi dogo linalopatikana Tanzania na duniani.
“Mzungu”, “western” kwa maana ya “wamagharibi” na neno kama “Kenyans”
kumaanisha uwepo wa Wakenya Loliondo ni baadhi ya maneno yanayojirudia rudia
midomoni mwao kama kauli mbiu ili kuwaudhi na kuwapandisha hasira waliowengi
pengine wajinga wakujitakia.
Manyerere anashindwa, labda kwa makusudi, hata kutaja
jina halisi la blog yangu, na kudai kwamba pengine ni tovuti, ambayo
imechapisha baadhi ya mada za blog yangu, yaweza kuwa ni ya kwangu. Hii ndio
Blog yangu: View from the Termite Mound.
Hii ni sehemu nzuri sana ya kupata habari zinazohusu uporaji wa ardhi ya wana
Loliondo unaofanywa na wawekezaji.
Na Susanna Nordlund
Kwa sasa nimetembelea Kenya na nategemea kurejea Tanzania
mwaka ujao
Hata baada ya kuchapisha kumjibu Manyerere kwa makala
yake aliyoiandika, bado amenitumia barua pepe ambayo ameambatanisha picha ya
akaunti yangu ya Facebook na ameandika hivi “You will never win this war!!”
kumaanisha kwamba “kamwe sitashinda hii vita" na hata nikamuuliza, “Nina
maelfu ya marafiki katika mtandao wa Facebook na wengi wao ni wafanyakazi wa
OBC kama wewe. Picha ile sio ya kificho kwa namna yeyote ile. Kitu gani
umezingatia kuona kwamba “umeshinda vita”? Au umeshinda kwa msingi kwamba
Wamasai wameondolewa kinyume na haki katika ardhi yao ya kilomita za mraba
1,500 na OBC kutumia haki ya uwindaji katika eneo hilo bila Wamasai? Au eneo la
kilomita za mraba 4,000? Au kwa kwa msingi kwamba bendera ya UAE inapepea
katika milingoti ya bendera za kitanzania?” Bado nasubiri majibu.
1 comment:
Post a Comment