Monday 11 July 2016

“Mwandishi” anayeihujumu Loliondo - Manyerere Jackton amkejeli tena Susanna Nordlund kwenye gazeti la Jamhuri


Mtafsiri: Innocent Zephania
Manyerere Jackton, ambaye mpaka sasa ameshaandika makala zaidi ya ishirini kuwatuhumu Wamasai wa Loliondo akidai kwamba ni waharibifu kutoka Kenya ambao asasi yao ya kiraia inawavuruga wawekezaji, hivi sasa ameandika tena kuhusu mimi… Ni Manyerere huyu huyu ambaye mwanzoni alikwenda mbali zaidi akidai kwamba zaidi ya asilimia 70 ya watu wa Loliondo ni ‘Wakenya’ na kwa kutaka kuthibitisha hilo, akachapisha orodha ya majina aliyodai ni ya ‘Wakenya’ hao. Msingi hasa wa makala yake, kabla ya hii ya sasa aliyoandika kuhusu mimi, makala aliyoiandika katika Gazeti la Jamhuri, June 15, 2016 yenye kichwa cha habari “Atuzwa kwa kuisumbua Serikali” (akiwa ameshirikiana na watu wawili wanaosadikika kuwa walarushwa wakubwa wa Loliondo) ni kutaka kumchafua mwanaharakati Maanda Ngoitiko tena kwa kutumia hoja za kizushi na za kuunganisha unganisha kuhusu namna ambavyo anadai nimefanya kazi chini ya asasi ya mwanaharakati huyu kitu ambacho sijawahi kufanya kwa namna yeyote ile, na hata kama ningekuwa nimeisaidia kwa namna nyingine, Je hilo sio jambo jema? Kilichotokea katika makala yake ya mwisho ni kwamba, Hashim Shaibu Mgandilwa - asiye na uadilifu, aliyekuwa mkuu wa wilaya - ni lazima angepokea maombi yangu kwa ufupi kuhusu kubatilisha hadhi ya marufuku ya kusafiri (prohibited immigrant status), kwa Waziri wa mambo ya ndani aliyejiuzulu Kitwanga kisha apeleke kwa mwandishi huyu anayeipinga Loliondo. Akiwa katika mtandao wa kijamii, kwa kejeli, Hashim Shaibu Mgandilwa akaniambia “nimesikia unataka unataka ku revoke PI njoo nikusaidie” na kwa muda mfupi sana baada ya kuniandikia hivyo, Manyerere Jackton naye akanitumia barua pepe ikiwa na ujumbe wa kitoto unaoishia na maneno haya “Finally, you will know who is the worst journalist and who is the worst mzungu!” kumaanisha kwamba “Mwishowe utapata kujua kwamba yupi ni mwandishi mbaya sana  na yupi ni mzungu mbaya sana” huku akiwa ameambatanisha na nakala ya barua yangu ya kwanza niliyowahi kutuma kuomba kubatilishiwa marufuku ya kusafiri (prohibited immigrant status). Angeweza kupata pia vielelezo vyangu vingine kuhusu maombi yangu kwa kina, lakini kwa kuwa ni mvivu pia au labda hakutaka basi hakuweza kufanya hivyo. Katika makala yake toleo la mtandaoni, makala ambayo haina hata jina la mwandishi - Manyerere alidai kwamba ni kutokana na “uchunguzi” uliofanywa na Gazeti la Jamhuri, hatimaye wamefichua hayo maombi yangu ya kutaka kubatilishiwa...


Ni jambo la kustaajabisha sana kuona kwamba, kwa nini Gazeti la Jamhuri linaendelea kuchapisha tuhuma za upotoshaji dhidi ya jamii ya Wamasai wa Loliondo ambao ni Watanzania. Kwa kumzingatia Manyerere binafsi, nimefikiri sana pengine atakua na mapungufu ya kisaikolojia, lakini kwa kuzingatia pia msingi wa niliyoyadadisi, inaonekana wazi kwamba mwandishi huyu anafadhiliwa na watu wa kitalu cha uwindaji cha OBC, watu wa ngazi ya juu kabisa wa jamii ya Falme za Kiarabu (UAE). Suala hili limejirudia rudia mpaka kupelekea serikali ya Tanzania kushawishika kutangaza uvamizi wa ardhi katika eneo hilo na mwaka 2009 ikawahamisha kwa nguvu, kutoka kilometa za mraba 1,500 (sehemu yote ni ardhi ya kijiji), bila hata ya ridhaa ya mahakama, Wamasai hao wa Loliondo. Kwa namna yeyote ile, makala ya hivi karibuni ya mwandishi huyu si ya kiuadilifu na imejaa simulizi za kizushi kwa nia ya kuudhi. Manyerere alipata pia kuandika bila weledi baada ya mimi kushikiliwa kinyume cha sheria nikiwa Loliondo kwa siku tatu bila ya kuruhusiwa kuwasiliana na mtu yeyote mnamo mwaka jana. Niliandika hivi katika blog baada ya kuachiwa huru.

Manyerere aliendeleza kutokuwa na weledi kwa kuandika kwamba nilikamatwa nikiwa napata chakula cha jioni katika hoteli aliyoitaja kwa jina la “Onesmo” hotel kitu ambacho sio kweli kwani hakuna hoteli yenye jina hili huku ilihali mimi nilikuwa katika nyumba ya kulala wageni ya ‘Honest Guest House’. Ijapukuwa ni dosari ndogo lakini ina msingi...

Manyerere alimtaja aliyekuwa Mkuu wa Wilaya (aliyehamishiwa Kigamboni) kama mtu ambaye amenifafanua mimi kuwa mdau mkuu katika kuiharibu Loliondo na Serengeti, na hii ikawajengea msingi…

Pia mwandishi huyu, anaikuza mada kwa hoja kwamba nilipata hifadhi Oloip, katika nyumba ya kulala wageni inayomilikiwa na aliyekuwa mbunge Mh Timan ambaye mke wake ndiye mwanaharakati pekee wa Loliondo ambaye ni mzaliwa wa Kenya, kitu ambacho kinamfanya mwanamama huyu kukosa nguvu kiasi kumpinga Manyerere. Ijapokuwa Manyerere hakufanikiwa sana kwa hilo kwa vile mwanamama huyo hana wadhfa tena wa udiwani wa CCM na mwaka jana kwenye uchaguzi, amechaguliwa Diwani wa viti maalumu wa Chadema. Manyerere aliendelea kudanganya kwamba nimeonekana kwenye mkutano wa siri huko Kirtalo nikiwa na Mh Tina Timan, japo nilishamfafanulia Manyerere kwa ufasaha kabisa mwaka jana kwamba si huyo mwanamama, bali ni watu wengine kabisa niliokutana nao huko Kirtalo nikiwa natimiza haki yangu ya msingi kama binadamu ya kukutana na watu wengine na kuchanganyika kwa hiari kwa ajili ya kutoa mawazo yangu hadharani.

Mwandishi huyu tena anarudia kupotosha kwamba nimekusanya “mabilioni ya fedha” kutoka katika mashirika ya kimataifa bila kuzingatia hoja kwamba sijawahi kuchangisha shilingi ya kitanzania. Labda abainishe wazi kwamba nani katika dunia hii amenipatia fedha. Kwa kuwa mwandishi huyu anaandika tu bila kuwa na mipaka ya kitaalamu, ni rahisi kwake kuandika chochote kile kuhusu uhatari wa wazungu na wamagharibi na kwa namna wanavyonimwagia fedha... Hupendelea kutumia muda mwingi kutunga uongo wa mimi na mambo ya fedha jambo ambalo linanifanya nifikiri sana kwamba pengine anafadhiliwa na OBC

Uongo mwingi ambao nimeshaukanusha tangu mwaka jana bado unarudiwa rudiwa, kama yale madai ambayo hayana maana ya kusema kwamba wakati niliposhikiliwa kinyume cha sheria, nilidai kwamba endapo serikali ya Tanzania itaendelea kunifuatafuata, nitahakikisha Sweden inakatisha misaada yake nchini. Manyerere anajua fika kwamba sikusema kitu kama hicho, na ni kwa sababu pia sina ushawishi katika hilo, lakini ni kitu tu ambacho “mwandishi” anapenda kukiandika. Kitu nilichowaambia wale mbumbumbu katika kituo cha polisi - wale wote isipokuwa mmoja, hawakujitambulisha kwangu, Mkuu wa Wilaya alikuwepo lakini nilimtambua - niliwaambia walipaswa kumshikilia pia meneja wa mashirika ya nje ambayo yanakiuka haki za ardhi - OBC kwa kuwa tishio dhidi ya kilomita za mraba 1,500, na pia Thomson Safaris - kutoka Marekani, kwa kuhusika na umiliki kinyume wa ekari 12,617, ardhi ya Wamasai. Watu wanaofichua ukweli kuhusu makampuni haya, si watu sahihi wa kukamatwa. Pengine ni Manyerere mwenyewe aliyetunga uongo huu au alitumia vyanzo vyake vya siri vya kimbumbumbu. “Majibizano” niliyoyapata kutoka kwa watu katika kituo cha polisi cha Loliondo ni kwamba “hakuna nchi katika dunia hii, mgeni anaruhusiwa kuzungumza siasa na watu” kauli inayoonyesha ujinga uliokithiri kuhusu haki za binadamu za msingi kama vile uhuru wa mtu kujieleza na kutoa maoni yake na uhuru wa kuchanganyika na watu kwa hiari.

Nimekua nikijihusisha na kuandika katika blog kuhusu uporaji wa ardhi unaofanywa na wawekezaji ndani ya Loliondo kwa takribani miaka sita sasa, sababu kubwa ikiwa kwamba nilikutana na mkasa ukaja ukazimwa kwa uongo na nikapata misukosuko wakati nilipokwenda Loliondo kuona kwa macho yangu mwenyewe. Sasa kama hakuna wa kushughulika nalo, nitafanya kila linalowezekana na kwa muda mrefu kama itakavyowezekana. Manyerere kwa upande mwingine anatumia nafasi katika gazeti la kitaifa, si tu kwa kumchafua mwanaharakati yeyote ambaye anaonekana kwenda kinyume na hawa wawekezaji, bali pia kuwabeza baadhi (asilimia 70) ya wakazi wa Loliondo. Anatumika kama silaha ya ukoloni mamboleo unaounga mkono uharibifu, suala ambalo ninalifichua na kulisemea kwa sasa. Dhana hii inajifafanua pia pale ambapo anatumia hata maneno ya kibaguzi kama “mzungu” yanayotumika mtaani, yeye huyatumia kwenye vichwa vya habari vya magazeti. “Kosa” kubwa analoweza kulibaini kwangu ni rangi yangu ambayo amekua akiitafakari kila mara huku akiwawezesha walioko nyuma yake kupaza sauti kuhusu nchi za magharibi asijue kwamba binafsi ninataka kuiimarisha nchi ya Tanzania kwa kuwaunga mkono wapigania haki ya ardhi ya Wamasai. Watanzania wengine wanaonishambulia kwa rangi yangu ni wale walioajiriwa na hawa wawekezaji waporaji wa ardhi, na wale wanaofurahia ubaguzi dhidi ya kundi dogo linalopatikana Tanzania na duniani. “Mzungu”, “western” kwa maana ya “wamagharibi” na neno kama “Kenyans” kumaanisha uwepo wa Wakenya Loliondo ni baadhi ya maneno yanayojirudia rudia midomoni mwao kama kauli mbiu ili kuwaudhi na kuwapandisha hasira waliowengi pengine wajinga wakujitakia.

Manyerere anashindwa, labda kwa makusudi, hata kutaja jina halisi la blog yangu, na kudai kwamba pengine ni tovuti, ambayo imechapisha baadhi ya mada za blog yangu, yaweza kuwa ni ya kwangu. Hii ndio Blog yangu: View from the Termite Mound. Hii ni sehemu nzuri sana ya kupata habari zinazohusu uporaji wa ardhi ya wana Loliondo unaofanywa na wawekezaji.

Na Susanna Nordlund
Kwa sasa nimetembelea Kenya na nategemea kurejea Tanzania mwaka ujao


Hata baada ya kuchapisha kumjibu Manyerere kwa makala yake aliyoiandika, bado amenitumia barua pepe ambayo ameambatanisha picha ya akaunti yangu ya Facebook na ameandika hivi “You will never win this war!!” kumaanisha kwamba “kamwe sitashinda hii vita" na hata nikamuuliza, “Nina maelfu ya marafiki katika mtandao wa Facebook na wengi wao ni wafanyakazi wa OBC kama wewe. Picha ile sio ya kificho kwa namna yeyote ile. Kitu gani umezingatia kuona kwamba “umeshinda vita”? Au umeshinda kwa msingi kwamba Wamasai wameondolewa kinyume na haki katika ardhi yao ya kilomita za mraba 1,500 na OBC kutumia haki ya uwindaji katika eneo hilo bila Wamasai? Au eneo la kilomita za mraba 4,000? Au kwa kwa msingi kwamba bendera ya UAE inapepea katika milingoti ya bendera za kitanzania?” Bado nasubiri majibu.

1 comment:

Apptians said...
This comment has been removed by a blog administrator.